DEREVA WA SUPER FEO MATATANI KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA AJALI: Dereva wa Kampuni ya mabasi ya Super Feo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyotokea leo, Jumapili asubuhi katika Kijiji cha Lilondo, Halmashauri ya Madaba wilayani Songea na kupelekea watu wawili kupoteza maisha. Akizungumza na AzamUTV kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio Kamanda wa Jeshi la Polisi, Saimon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali ya basi hilo lenye namba za usajili T-795 BKL aina ya Yutong lililokuwa na abiria 57. Kamanda Maigwa amesema kufuatia ajali hiyo watu 16 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini na hali zao zinaendelea vizuri na wengine wamesharuhusiwa kutoka. Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa ajali hiyo katika barabara ya kutoka Songea kuelekea Njombe ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa basi ambaye kwasasa anashikiliwa na jeshi hilo kusubiri uchunguzi kwa hatua za kumfikisha mahakamani. #ajali #majeruhi #basilaabiria #uzembe #Songea #usalama #polisi

Comments

Popular Posts